| Chapter 5 |
1 |
Kwa hiyo, mwigeni Mungu, maana ninyi ni watoto wake wapenzi.
|
2 |
Upendo uongoze maisha yenu, kama vile Kristo alivyotupenda, na kwa ajili yetu akajitoa mwenyewe kama dhabihu yenye harufu nzuri na tambiko impendezayo Mungu.
|
3 |
Kwa vile ninyi ni watu wa Mungu, basi uasherati, uchafu wowote ule au choyo visitajwe kamwe miongoni mwenu.
|
4 |
Tena maneno ya aibu, ya upuuzi au ubishi, yote hayo hayafai kwenu; maneno ya kumshukuru Mungu ndiyo yanayofaa.
|
5 |
Jueni wazi kwamba mwasherati yeyote au mchafu au mfisadi, (ufisadi ni sawa na kuabudu sanamu), au mtu yeyote wa aina hiyo hataambulia chochote katika Utawala wa Kristo na wa Mungu.
|
6 |
Msikubali kudanganywa na mtu kwa maneno matupu; maana, kwa sababu ya mambo kama hayo ghadhabu ya Mungu huwajia wote wasiomtii.
|
7 |
Basi, msishirikiane nao.
|
8 |
Zamani ninyi mlikuwa gizani, lakini sasa ninyi mko katika mwanga kwa kuungana na Bwana. Ishini kama watoto wa mwanga:
|
9 |
maana matokeo ya mwanga ni wema kamili, uadilifu na ukweli.
|
10 |
Jaribuni kujua yale yanayompendeza Bwana.
|
11 |
Msishiriki katika matendo yasiyofaa, ya giza bali yafichueni.
|
12 |
Mambo yanayotendwa kwa siri ni aibu hata kuyataja.
|
13 |
Lakini mambo yale yanayotendwa katika mwanga, ukweli wake hudhihirishwa;
|
14 |
na kila kilichodhihirishwa huwa mwanga. Ndiyo maana Maandiko yasema: "Amka wewe uliyelala, fufuka kutoka wafu, naye Kristo atakuangaza."
|
15 |
Basi, muwe waangalifu jinsi mnavyoishi: Msiishi kama wapumbavu, bali kama wenye hekima.
|
16 |
Tumieni vizuri muda mlio nao maana siku hizi ni mbaya.
|
17 |
Kwa hiyo, msiwe wapumbavu, bali jaribuni kujua matakwa ya Bwana.
|
18 |
Acheni kulewa divai maana hiyo itawaangamiza, bali mjazwe Roho Mtakatifu.
|
19 |
Zungumzeni kwa maneno ya Zaburi, nyimbo na tenzi za kiroho; mwimbieni Bwana nyimbo na zaburi kwa shukrani mioyoni mwenu.
|
20 |
Mshukuruni Mungu Baba daima kwa ajili ya yote, kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo.
|
21 |
Kila mmoja amstahi mwenzake kwa sababu ya kumcha Kristo.
|
22 |
Wake wawatii waume zao kama kumtii Bwana.
|
23 |
Maana mume anayo mamlaka juu ya mkewe, kama vile Kristo alivyo na mamlaka juu ya kanisa; naye Kristo mwenyewe hulikomboa kanisa, mwili wake.
|
24 |
Kama vile kanisa linavyomtii Kristo, vivyo hivyo, wake wawatii waume zao katika mambo yote.
|
25 |
Nanyi waume, wapendeni wake zenu kama Kristo alivyolipenda kanisa, akajitoa mwenyewe sadaka kwa ajili yake.
|
26 |
Alifanya hivyo, ili kwa neno lake, aliweke wakfu kwa Mungu, baada ya kulifanya safi kwa kuliosha katika maji,
|
27 |
kusudi ajipatie kanisa lililo takatifu na safu kabisa, kanisa lisilo na doa, kasoro au chochote cha namna hiyo.
|
28 |
Basi, waume wanapaswa kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. ((
|
29 |
Hakuna mtu yeyote auchukiaye mwili wake; badala ya kuuchukia, huulisha na kuuvika. Ndivyo naye Kristo anavyolitunza kanisa,
|
30 |
maana sisi ni viungo vya mwili wake.)
|
31 |
Kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: "Kwa hiyo, mwanamume atawaacha baba na mama yake, ataungana na mkewe, nao wawili watakuwa mwili mmoja."
|
32 |
Kuna ukweli uliofichika katika maneno haya, nami naona kwamba yamhusu Kristo na kanisa lake.
|
33 |
Lakini yanawahusu ninyi pia: kila mume lazima ampende mkewe kama nafsi yake mwenyewe, naye mke anapaswa kumstahi mumewe.
|